BONGO FLEVA : Akaunti ya Youtube ya Msanii Diamond platnumz wafungwa kwa kukiuka muongozo

BONGO FLEVA : Akaunti ya Youtube ya Msanii Diamond platnumz wafungwa kwa kukiuka muongozo

26 April 2022 0 By KAMIKAZI

Akaunti ya You Tube ya mwanamuziki maarufu kutoka Afrika Mashariki Diamond Platinumz imefungwa kwa kukiuka utaratibu na masharti ya mtandao huo.

Akaunti hiyo rilikuwa na wafuasi zaidi ya milioni 6 na video ambazo zimetazamwa na mamilioni ya watu.

Video yake maarufu aliyofanya na msanii kutoka Congo Dr Inno’s B ilikua na zaidi ya watazamaji milioni 100.

Kwa ujumla video zake zimetazamwa na watazamaji mara bilioni 1.

Sababu za kufungwa kwa mtandao zimeanishwa kuwa kukiuka masharti na sheria za mtandao.

Hatahivyo kwa mjibu wa meneja wa Diamond Hamisi Shaban Tale Tale amesema akaunt ya mnsanii huyo imechukuliwa na wadukuzi na hii ni mara ya pili kufanywa hivyo.

Diamond platnumz amekua ni msanii mwenye watazamaji wengi katika mtandao wa Youtube katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.

Facebook Comments Box
23430cookie-checkBONGO FLEVA : Akaunti ya Youtube ya Msanii Diamond platnumz wafungwa kwa kukiuka muongozo