Home ENTERTAINMENT BONGO FLEVA : Akaunti ya Youtube ya Msanii Diamond platnumz wafungwa kwa...

BONGO FLEVA : Akaunti ya Youtube ya Msanii Diamond platnumz wafungwa kwa kukiuka muongozo

396
0

Akaunti ya You Tube ya mwanamuziki maarufu kutoka Afrika Mashariki Diamond Platinumz imefungwa kwa kukiuka utaratibu na masharti ya mtandao huo.

Akaunti hiyo rilikuwa na wafuasi zaidi ya milioni 6 na video ambazo zimetazamwa na mamilioni ya watu.

Video yake maarufu aliyofanya na msanii kutoka Congo Dr Inno’s B ilikua na zaidi ya watazamaji milioni 100.

Kwa ujumla video zake zimetazamwa na watazamaji mara bilioni 1.

Sababu za kufungwa kwa mtandao zimeanishwa kuwa kukiuka masharti na sheria za mtandao.

Hatahivyo kwa mjibu wa meneja wa Diamond Hamisi Shaban Tale Tale amesema akaunt ya mnsanii huyo imechukuliwa na wadukuzi na hii ni mara ya pili kufanywa hivyo.

Diamond platnumz amekua ni msanii mwenye watazamaji wengi katika mtandao wa Youtube katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.

23431cookie-checkBONGO FLEVA : Akaunti ya Youtube ya Msanii Diamond platnumz wafungwa kwa kukiuka muongozo
Previous articleAUDIO | B Face Mkombozi Luxfer – Kimwe Ku Kindi | Download
Next articleINKURU ISHUSHE : Umuntu Umwe Yitavye Imana kubera Insanganya | Carama

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here