Dar Salam : Mzee Matata wa Mizengwe afariki

Dar Salam : Mzee Matata wa Mizengwe afariki

16 June 2021 0 By H. Mervis

Mchekeshaji kutoka kundi la Mizengwe Jumanne Alela (Mzee Matata) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taaarifa hizo zimethibitishwa na Mchekeshaji mwenzie wa Mizengwe Mkwere ambaye awali aliweka video akiwa analia kwenye ukurasa wake wa Instagram ambayo ilifuatiwa na post ya taarifa za kifo cha Mzee Matata.

June 13,2021 Katibu wa Chama Cha Waigizaji (TDFAA)- Wilaya ya Kinondoni alitoa taarifa ya kuugua kwa Mzee Matata ambayo ilielezea kuwa hali yake ni mbaya na amelazwa Muhimbili.

Taarifa ya Katibu ilisema “Mzee Matata hali yake mbaya alipelekwa Temeke Hospital kwa ajili ya matibabu kutokana na hali yake kahamishiwa Muhimbili ambapo alikuwa kalazwa mwanzo na kuruhusiwa juzi ila leo hali imebadilika ghafla kwa taarifa nilizopewa kakata kauli na ana kwikwi ya mfululizo DUA & SALA vinahitajika”

Facebook Comments Box
4860cookie-checkDar Salam : Mzee Matata wa Mizengwe afariki