Home NEWS R. Kelly awafukuza kazi Mawakili wake wawili

R. Kelly awafukuza kazi Mawakili wake wawili

311
0

Nguli wa muziki wa RnB Duniani, R. Kelly amewafuta kazi Mawakili wake wawili Steve Greenberg na Michael Leonard ikiwa ni miezi miwili kabla ya kesi  yake kusikilizwa.

Kupitia kikao kifupi na Mahakama mapema wiki hii Kelly ameeleza kuwa amewafuta kazi mawakili hao kwasababu hawakuwa vizuri kwenye suala la uwajibikaji na amepanga kuongeza timu ya wanasheria wapya ili kuziba nafasi hizo zilizoachwa wazi mapema kabla ya kesi yake.

R. Kelly amemthibitishia Jaji wa Mahakama Ann Donnelly kwamba ataendelea kufanya kazi na timu ya wanasheria wake Becker na Farinella ambao wamesalia kwenye ile timu ya watu wanne ili kushughulikia kesi yake inayomkabili ya unyanyasaji wa kingono.

4610cookie-checkR. Kelly awafukuza kazi Mawakili wake wawili
Previous articleVideo MPYA : Pechie B-Nation akuletea video mpya Lolo amshirikisha Alvin Smith |Download
Next articleVideo MPYA : Tomson The Voice ft B Face wakuletea hii “Umunoho” Itazame hapa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here